Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Etienne Ndayiragije amemuomba beki wa klabu ya Simba, Shomary Kapombe kutengua kauli yake ya kustaafu.

Siku kadhaa zilizopita Kapombe alitangaza maamuzi hayo magumu ya kuachana na Taifa Stars kutokana na majeraha ambayo amekuwa akisumbuliwa nayo.

Kapombe alieleza kuwa kwa sasa anhitaji kutulia ili kuilinda afya yake na akiitakia kila la kheri Stars ambayo bado inapigania nafasi ya kufuzu kuwania AFCON mwakani.

Kutokana na kujiengua, taarifa zimeeleza Ndayiragije amemuomba Kapombe kuitafakari upya kauli yake na maamuzi hayo kwani bado Stars inamhitaji.

Taarifa pia zinasema Ndayiragije ameamua kusema hayo akiamini Kapombe bado atakuwa na msaada mkubwa ndani ya kikosi hicho endapo akirejea kuendelea na kazi

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.