NAHODHA wa zamani wa Arsenal, Granit Xhaka amewaomba viongozi wa timu yake kukaa naye chini ili kuzungumza kuhusu mustakabli wake ndani ya timu hiyo kwa sasa kwa kuwa hawezi kusepa ndani ya timu hiyo kwa kuwa ana mkataba nao.

 Haya yote yametokea baada ya kupita kwa mwezi mmoja kwa nyota huyo kutoa lugha chafu kwa mashabiki wa Arsenal ambao walikuwa wanamzomea baada ya timu yake kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 na Crystal Palace wakati alipofanyiwa mabadiliko.

Kocha Mkuu wa Arsenal, Unai Emery aliamua kumvua unahodha na kumpatia nyota mwingine wa kikosi hicho Pierre Auba ambaye ndiye anaongoza jahazi kwa sasa na amesema kuwa hafikirii kama atamtumia nyota huyo kwenye kikosi chake kwa sasa.

Licha ya kuwepo kwa taarifa kwamba Xhaka mwenye umri wa miaka 27 ana mpango wa kusepa ndani ya Arsenal ameamua kuomba kuketi chini na klabu yake kwa kusema kuwa anahitaji kuzungumza nao kwa kuwa bado ana mkataba na timu yake hiyo.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.