Ripoti kutoka Congo ambako klabu ya TP Mazembe inatokea zinasema kuwa miamba hao wa soka nchini humo na Afrika wapo kwenye mchakato wa kujenga uwanja mpya.

Inaelezwa uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuingiza jumla ya watu ama zaidi ya watu 50,000.

Taarifa zinasema kuwa Rais wa klabu hiyo, Moyes Katumbi, ametangaza kuanza kuwa Mazembe itajenga kiwanja hicho ambacho kitakuwa ni moja ya viwanja vikubwa nchini Congo.

Maamuzi hayo yamekuja kufuatia Mazembe itakuwa inatimiza miaka 80 tangu kuanzishwa kwake.

Maamuzi ya Mazembe ni sawa na wanachokifanya Simba kwa sasa ambao wanaelekea kukamilisha uwanja wa mazoezi kabla ya kuanza kujenga majukwaa hapo baadaye pamoja na Yanga ambao wameshaanza kuandaa uwanja wao Kigamboni, Dar es Salaam.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.