Licha ya kupapaswa kwa jumla ya mabao 3-0 dhidi ya Simba, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amewaponda wapinzani wake.

Masau amesema kuwa Simba hawakucheza mchezo mzuri na hata mabao yao yalikuwa hayana mipango.

Ikumbukwe Masau awali alitamba kuwa jana ingekuwa zamu ya Simba kula kichapo baada ya kuzifunga timu za Azam FC, Yanga na KMC.

Ushindi huo ulizidi kuwafanya Simba warejee kileleni kwa kufikisha jumla ya alama 25 ikiwa imecheza mechi 10.

"Hakuna mpira wa maana walioucheza Simba, mabao yao yalikuwa hayana mipango, yalikuwa mepesi mno, tofauti na sisi tuliocheza soka safi," amesema Masau.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.