Timu zote nne zinaweza kufuzu katika awamu ya muondoano katika kombe la vilabu bingwa wiki hii.
Nafasi tatu tayari zimenyakuliwa na kuna nyengine 13 zilizosalia.
Bayern Munich, Juventus na Paris St- Germain ni timu ambazo tayari zimefuzu katika kundi la timu 16 huku zikiwa zimesalia na mechi mbili kucheza.
- Liverpool washinda kombe la UEFA Champions League
- Samatta aweka historia, Genk yaadhibiwa Champions League
- Mourinho aivulia kofia Juventus
Haya ndio mahitaji ya klabu za Uingereza ili kuweza kusonga mbele:
- Tottenham: itasonga mbele kutoka kundi B iwapo itaishinda Olympiakos siku ya Jumanne , ama iwapo watapata sare huku klabu ya Red Star Belgrade ikifeli kuishinda Bayern Munich.
- Manchester City: Ushindi dhidi ya Shakhtar Donetsk siku ya Jumapili itaiweka City kuwa washindi wa kundi C. Sare itawahakikishia wanasonga mbele katika kundi la timu 16.
- Liverpool: Ushindi dhidi ya Napoli siku ya Jumatano utaiweka ljuu kama washindi wa kundi E . Iwapo Salzburg itashindwa kuilaza Genk, Liverpool itasonga mbele licha ya matokeo yake dhidi ya Napoli
- Chelsea: Itasonga mbele kutoka kundi H ikipwa itapata ushindi dhidi ya Valencia kwa kuwa watakuwa na rekodi nzuri dhidi ya klabu hiyo ya Uhispania.
Kundi A
Mabingwa wa Ligue 1 PSG wamesonga mbele katika kundi A wakiongoza kundi hilo baada ya kushinda mara nne. wamefunga magoli 10 na bado hawajafungwa.
Real Madrid ambao ndio washindi mara 13 wa mashindano hayo , wako katika hali nzuri ya kusonga mbele pointi tano ya klabu ya Ubelgiji ya Bruges ambayo ipo katika nafasi ya tatu.
Mabingwa wa Uturuki galatasaray wameondolewa.
Mechi zilizosalia:
Jumanne , 26 Novemba - Galatasaray v Bruges, Real Madrid v PSG
Jumatano, 11 Disemba - PSG v Galatasaray, Bruges v Real Madrid
Kundi B
Mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich walisonga mbele kutoka kundi B wakishinda mara nne katika mechi nne.
Msimu uliopita Tottenham ambayo ilishindwa katika fainali itasonga mbele iwapo itaishinda Olympiakos siku ya Jumanne, ama iwapo watatoka sare na Red Star Belgrade itafeli kuishinda Bayern Munich. Olympiakos wako chini wakiwa na pointi moja na watahitaji matokeo kuwapendelea ili kusonga mbele.
Mechi zilizosalia:
Jumanne, tarehe 26 Novemba - Tottenham v Olympiakos, Red Star Belgrade v Bayern Munich
Jumatano, tarehe 11 Disemba - Bayern Munich v Tottenham, Olympiakos v Red Star Belgrade
Kundi C
Mabingwa wa ligi ya Premia Manchester City walikosa fursa ya kujumuika katika timu 16 bora kwa kutoka sare ya 1-1 dhidi ya klabu ya Atalanta iliopo chini ya kundi C , ambao huenda wakasonga mbele iwapo watashinda mechi zote mbili zilizosalia.
Klabu ya Pep Guardiola inahitaji pointi moja ili kuhakikisha wanasonga mbele. Shakhtar Donetsk na Dinamo Zagreb walio katika nafasi ya tatu wako na pointi tano kila mmoja.
Mechi zilizosalia:
Jumanne, tarehe 26 Novemba - Manchester City v Shakhtar Donetsk, Atalanta v Dinamo Zagreb
Jumatno, tarehe 11 Disemba - Shakhtar Donetsk v Atalanta, Dinamo Zagreb v Manchester City
Kundi D
Mbingwa wa serie A Juventus walitoka nyuma na kuishinda Lokomotiv Moscow 2-1 na kusonag mbele katika kundi D wakiwa na pointi 10 kutoka katika mechi nne.
Klabu ya Atletico madri ambayo ipo katika nafasi ya nne iki pointi nne juu ya Lokomotiv na Bayer Leverkusen ambao wote wana pointi tatu.
Mechi zilizosalia:
Jumanne, tarehe 26 Novemba - Lokomotiv Moscow v Bayer Leverkusen, Juventus v Atlético Madrid
Jumatano, tarehe 11 Disemba - Atlético Madrid v Lokomotiv Moscow, Bayer Leverkusen v Juventus
Kundi E
Mabingwa watetezi Liverpool wanaongoza kundi E na ushindi mmoja kutoka katika mechi mbili za mwisho walizocheza itazipeleka kusonga mbele katika kundi la timu 16.
Napoli ambayo ipo katika nafasi ya pili ina pointi nane , ikiwa ni nne zaidi ya klabu ya Red Bull Salzburg , huku Genk wakiondolewa kwa kuwa wana pointi moja pekee.
Mechi zilizosalia:
Jumatno tarehe 27 Novemba - Liverpool v Napoli, Genk v Red Bull Salzburg
Jumanne , tarehe 10 Disemba - Napoli v Genk, Red Bull Salzburg v Liverpool
Kundi F
Mabingwa wa La Liga Barcelona watasonga mbele katika kundi F iwapo wataishinda Borussia Dortmund katika mechi yao itakayochezwa katika uwanja wa Nou Camp .
Timu hiyo ya Ujerumani ilipata ushindi wa 3-2 dhid ya Inter Milan kutoka 2-0 nyuma ambao ulikuwa muhimu huku wakisalia pointi tatu nyuma dhidi ya timu hiyo ya Itali. Slavia Prague iko chini katika jedwali.
Mechi zilizosalia:
Jumatano tarehe 27 Novemba - Barcelona v Borussia Dortmund, Slavia Prague v Inter Milan
Jumanne tarehe 10 Disemba - Borussia Dortmund v Slavia Prague, Inter Milan v Barcelona
Kundi G
RB Leipzig inaongoza katika kundi G na inahitaji ushindi mmoja kutoka kwa mechi zake mbili zilizosalia ili kusonga mbele.
Post a Comment