KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngasa amesema kuwa kwa sasa atafunga kila anapopata nafasi ndani ya timu yake kwa ajili ya kurejesha heshima ndani ya ligi.
Ngasa ambaye alijiunga na Yanga msimu wa 2018/19 akitokea Ndanda FC ya Mtwara baada ya kuikoa isishuke daraja ametupia bao moja ndani ya Yanga pamoja na asisiti moja kwenye ligi ametuma salamu hizo kwa JKT Tanzania itakayoshuka uwanjani kesho.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ngasa amesema kuwa kwa sasa ligi bado mbichi na timu yake ina mechi nyingi hivyo mashabiki wanapaswa waendelee kutoa sapoti kwa Yanga kwani kazi bado inaendelea.
“Kufunga ni sehemu ya matokeo na mipango ya kila mchezaji kwani ili timu ishinde ni lazima mabao yapatikane, kwa sasa tuna kazi kubwa ndani ya ligi ukizingatia kwamba kila timu ipo vizuri.
“Mashabiki waendelee kutupa sapoti kwani wamekuwa nasi bega kwa bega hata kwenye mchezo wetu wa kirafiki dhidi ya Coastal Union wengi walijitokeza ni furaha kwetu nasi tunajivunia uwepo wao,” amesema Ngasa.
Kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Taifa, Ngassa alifunga bao akiwa nje ya 18 kwenye ushindi wa mabao 3-1 kwa sasa timu yake ipo nafasi ya15 kwenye ligi imecheza mechi tano pekee na ina pointi 10 pekee
Post a Comment