Akizungumza na wandishi wa Habari ofsini kwake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ulrich Matei alisema Julius alikamatwa Novemba 20 mwaka huu katika eneo la Mafiati jijini Mbeya akiwa na Kete 27 za dawa hizo alizohifadhi kwenye mfuko wa suruali.
Alisema baada ya kumhoji alisema dawa hizo sio zake bali ni za rafiki yake ajulikanaye kwa jina la Kelvin Mwankuga (28) mkazi wa Kata ya Mwakibete jijini Mbeya na walianza kumtafuta na kumkamata akiwa nyumbani kwake Novemba 21 mwaka huu.
Kamanda alisema wanaendelea kuchunguza tukio hilo na watuhumiwa watafikishwa mahakamani hivi karibu kujibu tuhuma zinazowakabili.
Post a Comment