HASSAN Mwakinyo, bondia wa ngumi za kulipwa jana ametangaza wazi kuwa ameamua kufanya bure pambano lake la kimataifa dhidi ya Mfilipino, Arnel Tinampay.
Pambano hilo la raundi kumi ambalo halitokuwa la ubingwa linatarajia kufanyika Novemba 29, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar.
Mwakinyo amesema hayo katika onyesho la wazi kwa ajili ya kutambulisha pambano ‘Face Off’ iliofanyika kwenye Viwanja wa Leaders jijini Dar kuelekea kwenye pambano hilo la kukata na shoka.
Mwakinyo amesema kuwa ameamua kufanya hivyo kwa lengo la kuendelea kuhamasisha mchezo huo ambao umeanza kupotea umaarufu wake huku akitamba kumpoteza Mfilipino katika pambano hilo.
“Kwanza nataka niwaambie Watanzania wote kwamba tumeamua kufanya pambano hili bure baada ya kukubaliana na hili limefanyika kwa maslahi mapana ya mchezo wenyewe, hivyo kikubwa tunawaomba wadau kujaza uwanja siku hiyo ili niweze kushinda kwa kuwa najua hatoweza kutoka,” amesema.
Kwa upande wa Tinampay anayetoka kwenye kambi ya bondia bora duniani, Manny Pacquao amesema kuwa amekuja nchini kwa kazi moja tu ya kuhakikisha anamchakaza vibaya Mwakinyo katika pambano hilo huku akifurahishwa na ukarimu wa Watanzania katika sehemu zote alizotembelea
Post a Comment