Imeelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Simba umeibuka na kusema watani zao wa jadi Yanga ndiyo wamekuwa wakisambaza taarifa za Kocha Patrick Aussems kufukuzwa kazi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa katika kurasa za mitandao ya kijamii ya Radio EFM, imesema Simba wameeleza Yanga ndiyo wamekuwa wakisambaza taarifa hizo ambazo hazina ukweli.

Uongozi wa Simba umefunguka kuwa Aussems amesafiri kuelekea kwao Ubelgiji kwa ajili ya mambo ya kifamilia na anatarajiwa kurejea leo nchini.

Kocha huyo anatajwa kurejea leo ili kuendelea na majukumu ya kazi kuelekea mechi ya ligi na Ruvu Shooting

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.