Lipuli wanaangalia uwezekano wa kuwachukua wachezaji wawili wa Simba kwa mkopo Yusuph Mlipili pamoja na Kennedy Juma katika usajili wa dirisha dogo utakaofunguliwa Desemba 16, mwaka huu.
Lipuli imejipanga kuhakikisha inafanya vizuri katika ligi msimu huu ambapo katika ligi hiyo Lipuli wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 18 nyuma ya Kagera Sugar na vinara Simba.
Ofisa Habari wa Lipuli, Clement Sanga, alisema; “Tunaamini wataongeza kitu eneo la ulinzi maana katika ushambuliaji tupo vizuri.”
Mlipili na Kennedy wote kwa pamoja wameshindwa kuwa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kwa muda sasa ambapo katika nafasi yao Simba imekuwa ikiwatumia zaidi Erasto Nyoni, Pascal Wawa na Mbarazili Tairone Santos
Post a Comment