Kuna uwezekano mkubwa beki wa Yanga Andrew Vincent 'Dante' akaondoka ndani ya kikosi cha Yanga kutokana na kutokuwa kwenye maelewano na mabosi wa klabu hiyo.
Kutoelewana kwa Yanga na Dante kunatokana na madai ya fedha za mchezaji huyo ambazo ni zaidi ya milioni 45 za kitanzania ambazo zilimfanya agome kucheza tangu mwanzo mwa msimu huu.
Dante aligoma kucheza Yanga akishinikiza alipwe kwanza fedha zake na kuelekea mwishoni mwa msimu huu kuna uwezekano akasajiliwa na timu nyingine sababu mkataba wake utakuwa umemalizika.
Taarifa zilizopo zinasema endapo Yanga wakimlipa fedha hizo anaweza akaanza mzungumzo na timu nyingine kwa ajili ya kwenda kuitumikia baada ya kutokuwa na furaha na mabosi wa Yanga kwa namna walivyoshindwa klipa stahiki zake hadi leo.
Ikumbukwe Dante kabla hajatua Yanga ambayo haijachukua ubingwa wa ligi misimu miwili iliyopita, awali alikuwa akiicheza Mtibwa Sugar ya Morogoro
Post a Comment