UONGOZI wa Tottenham umempiga chini mazima aliyekuwa kocha wao kwa muda wa miaka mitano ndani ya klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England Mauricio Ponchettino.

Pochettino ameiongoza timu yake hiyo ikiwa nafasi ya 14 kwenye Ligi kuu ikiachwa kwa jumla ya pointi 20 na vinara ambao ni Liverpool kwa sasa.

Timu hiyo msimu huu imeshinda mechi tatu pekee jambo ambalo limewafanya mabosi hao kuhofia kushushwa daraja ndani ya Ligi Kuu England.

"Timu imeamua kuachana na Pochettino ndani ya timu pamoja na benchi lake la ufundi ikiwa ni pamoja na Jesus Perez, Miguel D'Agostino na Antoni Jimenez," imeeleza taarifa hiyo

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.