Mlinda mlango wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Juma Kaseja amemkingia kifua nahodha na mshambuliaji wa timu hiyo Mbwana Ally Samatta kwa kusema hakuna haja kwa mashabiki kumbebesha mzigo wa lawama, kufuatia matokeo mabaya ya kufungwa mabao mawili kwa moja dhidi ya Libya, Juzi Jumanne.

Kaseja amechukua maamuzi hayo alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya timu kuwasili leo alfajiri jijini Dar es salaam, kwa kusema haoni kama ni jambo sahihi kwa mashabiki kumtuhumu Samatta kwa kilichoonekana kupitia mchezo dhidi ya Libya.

Mlinda mlango huyo mkongwe amesema, lawama za matokeo mabaya zinapaswa kuelekezwa kwa wachezaji wote wa Taifa Stars, ambao walikuwa ndani na nje ya uwanja.

“Sioni kama ni jambo sahihi, imepoteza timu nzima, isitoshe Samatta ana mchango mkubwasana kwenye kikosi cha Stars, na kama juzi hakua vizuri tutambue naye ni binadamu, huwezi kujua nini kilimkuta,” alisema.

Mbali na hilo akasema licha ya kupoteza kwa mabao mawili kwa moja  dhidi ya Libya sio mwisho Taifa Stars, bali anaamini Tanzania ina nafasi kubwa ya kufanya jambo kwenye michezo ijayo ya kundi J.

“Ni kweli tunakubali kupokea lawama ingawa hatupendezwi na hali hiyo, ila ni vyema kuheshimu matokeo ya soka, kocha alitumia mipango yake lakini kwa bahati mbaya mambo yalikwenda tofauti,”

Kaseja amesema walijipanga kulingana na mchezo husika “Lazima tufanye maandalizi kulingana na timu ambayo tunakwenda kucheza nayo, tumeteleza sasa tuungane kwa pamoja tuangalie mbele,” alisema mkongwe huyo.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.