Ijumaa ya wiki iliyopita kiungo Jonas Mkude alichelewa mazoezi ya timu hiyo yaliyokuwa yakifanyika Viwanja vya Gymkhana, Posta, Dar sasa jana tena mchezaji huyo amerudia ya wiki iliyopita. Mkude ambaye ni kati ya viungo wakabaji bora Bongo, ndiye mchezaji mkongwe Simba ambako ndipo alipoanzia soka lake.

Sasa twende mazoezini; wiki iliyopita uwanja uleule, tabia ileile ya kuchelewa aliionyesha ambapo alifika mazoezini wakati wenzake wameshafanya kwa zaidi ya dakika 15 tena akiwa ndani ya ndinga kali aina ya Toyota Harrier.

Alipofika tu, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemanu alionekana kuchukizwa na kitendo cha Mkude kisha akamuonya kwa kumtaka kutorudia tena.

Sasa juzi Ijumaa, kwa mara nyingine Mkude alifika mazoezini na kukuta wenzake wanaelekea kumaliza mazoezi, akapaki gari yake aina ya Toyota Harrier huku akiwa amevalia kaptura ya jinzi iliyochanwa kisasa kwenye mapaja na juu alivalia fulana nyeusi.

Wakati akiingia uwanjani hapo, meneja alionekana akimuagiza mpiga picha wa timu hiyo ampige Mkude kama ushahidi. Moja kwa moja alikwenda kuonana na Rweyemamu kisha kocha wa viungo, Adel Zrane, hawa wote walionekana kutofurahishwa na kitendo hicho.

Rweyemamu aliliambia Championi Jumamosi kuwa, Mkude atajadiliwa kwenye kikao cha viongozi wa Simba chini ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Senzo Mazingiza ambaye ni raia wa Afrika Kusini. Ikumbukwe Mkude aliachwa katika michezo miwili iliyopita dhidi ya Singida United na Mwadui FC kutokana na kutokuwa sawa kimwili.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.