Wakongwe Yanga kwa kushirikiana na kampuni ya GSM, leo wametambulisha jezi rasmi za timu hiyo watakazozitumia msimu wa 2019/20.

Hafla hiyo ya utamburisho wa jezi hizo mpya ilifanyika leo asubuhi kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dr Mshindo Msolla alisema kuwa hizo ndiyo jezi rasmi na halari za Yanga watakazozitumia katika msimu ujao.


Msolla alisema kuwa, jezi hizo zina ubora mkubwa kutokana utengenezwaji wa walioshinda tenda hiyo ambao ni GSM zitakazopatikana maduka ya GSM Msasani Mall, Pugu Mall na Makao Makuu ya Yanga.


"Hakuna jezi yenye ubora kama huu nchini Tanzania. Pia tutafungua duka kubwa la vifaa mbalimbali vyenye nembo ya Yanga, hamjawahi kuona duka la Kimataifa kama hilo," alisema Msolla.



Mkurugenzi wa GSM, Hersi Said alisema kwa upande wake alisema kuwa “Hakuna jezi yenye ubora kama huu tuliouzindua leo hapa nchini, baada ya uzinduzi huo tutafungua duka kubwa la vifaa mbalimbali vyenye nembo ya Yanga ambalo halijawahi kutokea.

Tags:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.