MSHINDO Msolla, mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa mashabiki wa Yanga wanunue kwa wingi jezi halisi ambazo zimezinduliwa leo kwa manufaa ya klabu.

Msolla amesema:"Wakati nazunguka kwenye matawi mashabiki na wanachama walikua wananiambia hawataki kununua jezi kwasababu club hainufaiki. Sasa nawambia wanunue kwa sababu club inanufaika.

"Hakikisha unanunua jezi halisi. Tayari zimeanza kuuzwa kwenye maduka ya GSM Msasani Mall, Pugu Mall na makao makuu ya Yanga.


Nayo waliotengeza jezi hizo kampuni ya GSM kupitia mwakilishi wao wamesema:-
"Hakuna jezi yenye ubora kama huu tutakao zindua leo nchini Tanzania. Pia tutafungua duka kubwa la vifaa mbalimbali vyenye nembo ya Yanga.Hamjawahi kuona duka la Kimataifa kama hilo."
Tags:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.