MPANGO wa nyota wa timu ya Everton kutimkia Paris Saint Germain umemfanya awe na furaha muda wote Kwa sasa.
Gueye mwenye umri wa miaka 29 amejiunga na mabingwa wa Ligue 1 kwa mkataba wa miaka minne.
Nyota huyo anayekipiga timu ya Taifa ya Senegal sasa atakuwa naye ndani ya kikosi cha mabingwa hao.
"Baada ya kurejea kwenye michuano ya Afcon, nilikuwa nataka nipate changamoto mpya na nilipokuwa nikihusishwa na PSG sikuwa na mashaka kwani ni timu yenye mipango Bora.
"Ni furaha kwangu kutimiza ndoto zangu, ilikuwa sehemu ya mipango yangu," amesema Idrissa Gueye nyota mpya wa PSG kutoka Everton.
Imeripotiwa kuwa dau lake la uhamisho ni Euro milioni 32.
Post a Comment