KARIOBANGI Sharks, wababe wa kikosi cha Everton ambacho kinadhaminiwa na SportPesa tayari wapo ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Yanga.
Kariobangi Sharks itamenyana na Yanga uwanja wa Taifa mchezo wa kirafiki ambao ni maalumu kwa ajili ya kutambulisha wachezaji wa Yanga pamoja na jezi mpya zitakazotumika msimu wa mwaka 2019/20.
Awali Yanga ilipanga kucheza na AS Vita kutoka Congo mipango ilibadilika baada ya ratiba ya michuano ya kimataifa kutolewa jambo lililowafanya AS Vita kushindwa kuja.
Everton wanawatambua Kariobangi Sharks baada ya kufungwa kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Kenya baada ya kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 dakika tisini ilipoteza kwa kufungwa penalti 4-3.
Post a Comment