OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa mashabiki wa Simba wasisahau kujitokeza kwa wingi Agosti 6 uwanja wa Taifa.
Simba kwa sasa ipo kwenye SpotiPesa Simba Wiki, ambayo kilele chake ni Agosti 6 uwanja wa Taifa na itacheza mchezo wa kirafiki na Power Dynamo.
Siku hiyo itakuwa rasmi kwa ajili ya kutambulisha jezi mpya za Simba, vifaa vya michezo, nyimbo maalumu ya Simba pamoja na wachezaji wote waliosajiliwa na Simba.
"Ni siku nzuri na imepangiliwa kwa uzuri kabisa kuanzia matukio na mambo yote uwanja wa Taifa, mashabiki ni wajibu wenu kuipa sapoti timu yenu ya Simba.
"Kutakuwa na burudani za kutosha hivyo haya yote yameandaliwa kwa ajili ya mashabiki na wapenzi wa Simba,kama kawaida yetu ilivyo kuujaza uwanja tunapaswa tuweke rekodi mpya ili na ule uwanja wa Uhuru tuweke screen kubwa" amesema.
Katika kuadhimisha SportiPesa Simba Wiki wamekuwa wakitembelea hospitali mbalimbali na kuwaona wagonjwa pamoja na kujitolea damu.
Post a Comment