MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ni wakati wa mashabiki kujitokeza kwa wingi leo uwanja wa Taifa kushuhudia namna timu itakavyofanya maajabu.
Leo ni kilele cha siku ya Mwananchi ambapo Yanga itacheza mchezo wa kirafiki na Kariobangi Sharks ya Kenya.
Zahera amesema: "Inafaa kila mwanachama na shabiki wa Yanga kujitokeza kuona namna gani timu imejiandaa kwa ajili ya msimu ujao pamoja na kuwaona wachezaji wake wapya.
"Maandalizi kuhusu wachezaji pamoja na hali zao kwa pamoja zipo sawa hivyo ni suala la muda tu kwa wachezaji kutoa burudani kwa mashabiki," amesema.
Leo kuanzia saa nne uwanja wa Taifa utakuwa wazi kwa ajili ya kuhitimisha kilele cha wiki ya Mwananchi ambapo Yanga itawatambulisha wachezaji wake pamoja na jezi za msimu mpya wa 2019/20.
Post a Comment