SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeanza mchakato wa kupunguza timu zinazoshiriki ligi kuu Soka Tanzania bara mpaka kufikia timu 16.
Kupitia ukurasa maalumu wa Shirikisho hilo kwenye mtandao wa Twitter TFF imeandika "Tumepanga kupunguza timu kutoka timu 20 msimu huku mpaka timu 16 msimu wa mwaka 2021/2022, hii ni baada ya kufanya tathmini ya kina juu ya ligi yetu".
Timu 20 ziliongezwa na TFF msimu wa mwaka 2018/19 ambapo Ligi ilimalizika bila ya kuwa na mdhamini mkuu.
Post a Comment