JOHN Bocco, nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' amesema kuwa imani kubwa kwa sasa ni kupata matokeo chanya mbele ya Kenya.

Stars ipo Kenya kwa ajili ya mchezo wa marudio dhidi ya Kenya utakaochezwa Agosti 4 na ili kusonga mbele kwenye michuano ya Chan ni lazima Stars kupata ushindi ikiwa ni baada ya kupata sare ya bila kufungana uwanja wa Taifa.

"Makosa ambayo tulifanya awali tayari benchi la ufundi limeyafanyia kazi hivyo imani yetu ni kupata matokeo chanya.

"Shukrani kwa mashabiki kwa sapoti zao tunatambua namna ambavyo wapo nasi hivyo nasi tutapambana kusonga mbele kwenye michuano hii," amesema.

Tags:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.