HARRY Maguire anatajwa kuja kuwa mchezaji ghali duniani baada ya Manchester United kukubali kuweka mzigo wa pauni milioni 85 kukamilisha dili hilo kumchukua kutoka Kwa Leicester City.
United msimu uliopita wa Ligi Kuu England iliruhusu jumla ya mabao 53 na ilitupwa nje na Barcelona kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Ole Gunnar Solskjaer, Meneja wa United amemchambua beki huyo Kwa kusema kuwa ni chaguo lake msimu huu baada ya kuanza na Aaron Wan-Bissaka ambaye aligharimu pauni milioni 50.
Kutokana na Erick Bailly kusumbuliwa na majeraha huku Marcos Rojo akiwa yupo nje ya mpango wake Solskjaer anaamini ataongeza nguvu ndani ya kikosi.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 anatarajiwa kukamilisha taratibu zote wikendi kabla ya kutua ndani ya Old Trafford.
Post a Comment