HAJI Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa uongozi wa Simba una imani na mashabiki wake hasa linapokuja suala la kuujaza uwanja wa Taifa wakati timu inacheza mechi yoyote ile.
Simba kwa sasa ipo kwenye SpotiPesa Simba Wiki, ambayo kilele chake ni Agosti 6 uwanja wa Taifa na itacheza mchezo wa kirafiki na Power Dynamo.
Manara amesema:"Linapokuja suala la mashabiki wa Simba kujitokeza uwanja wa Taifa na kuujaza kabisa mwanzo mwisho hilo halihitaji kelele, wenyewe wanajua wajibu wao na ni jadi yetu.
"Mashabiki wa Simba wanapenda kuona timu inafanya vizuri, wanapenda kuona wachezaji wanajituma hivyo furaha ya mashabiki wao ni kuwa uwanjani kuisapoti timu suala la Agosti 6 ni kusubiri na kuona.
"Mashabiki wa Simba wanaipenda timu yao wapo bega kwa bega hivyo tunawaomba hilo walitambue jadi yao ya kuisapoti timu iendelee, tuujaze uwanja wa Taifa," amesema.
Post a Comment