KAZI kubwa imebaki kwa timu ya Taifa ya Tanzania kupata matokeo mbele ya Kenya nchini Kenya kwenye mchezo wa marudio ya kufuzu kupata nafasi kushiriki michuano ya Chan.

Matarajio ya awali ilikuwa ni kuona timu inapata matokeo kwenye mchezo wa kwanza nyumbani kisha safari ya Kenya hesabu zilikuwa ni kwenda kukamilisha ratiba.

Mwisho wa siku kinachotokea ndicho tunachokipokea kwani Mungu anapanga na binadamu anapanga pia ni matokeo yetu tunayachukua na kuyafanyia kazi.

Kumaliza dakika 90 bila kufunga bao nyumbani ni matokeo ambayo kwa kiasi fulani yanawavunja moyo watanzania kwa kushusha ile imani yao kwa timu ya Taifa.

Ila bado ninaona kuna nafasi ya kupata matokeo ugenini pia licha ya kushindwa kufanya vizuri nyumbani mchezo wa kwanza.

Tusisahau kwamba kambi ya timu ya Taifa imeundwa kwa muda mfupi na matokeo tumeyaona namna wachezaji walivyojituma kwa juhudi na kwa bidii kusaka ushindi.

Mwisho wa siku tunaona kwamba sare imetuweka hapa na tunaanza safari nyingine kuifuata Kenya kwa ajili ya kupambana zaidi.

Kwenye maisha ya soka hakuna ambacho kinashindikana na hakuna ruhusa ya kukata tamaa licha ya ushindani kuwa mkubwa kikubwa ni kuungana.

Wachezaji wanajua namna walivyopambana na makubaliano ya kusaka ushindi ndani ya ardhi ya nyumbani hivyo kushindwa kutimiza hesabu za mwanzo maana yake kazi mpya inaongezeka.

Kwa sasa watanzania wanapaswa waendeleze ule muungano na ushirikiano kwani kazi bado inaendelea na hakuna ambaye amemaliza safari ndo kwanza mgawanyiko wa kwanza umekwisha.

Dakika 90 za kwanza zimekamiilika zimebaki dakika 90 nyingine za ugenini ambazo zitakuwa ni za machozi na damu katika kutafuta ushindi bado nafasi ipo.

Uwezekano wa kutimiza lile lengo la Taifa kufuzu michuano ya Chan bado ipo mikononi mwa wachezaji wenyewe ndani ya uwanja.

Kilichobaki ni kwa mashabiki kuipa sapoti timu ya Taifa licha ya kuona kwamba imeshindwa kupata matokeo.

Kuikatia tamaa sio jambo jema kwani linaimaliza moja kwa moja timu yetu ya Taifa ambayo kwa sasa haipo sehemu mbaya kupata matokeo.

Wao wameweza kulazimisha sare nyumbani kwetu basi nasi pia tuna nafasi ya kulazimisha kupata matokeo nyumbani kwao jambo litakaloongeza furaha ya kweli.

Matokeo ambayo yametokea hatuna uwezo wa kuyabadili kwa sasa zaidi ya kujipanga upya kwenda kumaliza kazi ambayo tumeianza na kwa juhudi kubwa.

Mashabiki wengi waliojitokeza uwanja wa Taifa ni jambo la uzalendo hivyo ndivyo inatakiwa kuwa siku zote mshikamano ni kitu cha msingi yanapofika 

masuala ya kupambana kwa ajili ya Taifa.

Vijana wamekaa muda mfupi na wameweza kupambana kwa kiasi kile imani kubwa ni kwamba kama wakipata nafasi nyingine ya kuaminiwa lazima wataitumia vizuri.

Mashabiki msiwavunje moyo vijana kwa kuwa safari bado inaendelea na wahenga walisema kuwa kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi .

Bado kwa sasa kuna nafasi ya kufanya vema na kupenya mpaka Cameroon mwaka 2020 kushiriki michuano ya Chan ni suala la kusubiri muda na kuendelea kutoa sapoti katika kila jambo.

Taifa letu la Tanzania lina vipaji vingi na wengi wanajua kucheza mpira hivyo ni suala la kusubiri na kuona.

Makosa ya vijana ni sehemu ya mpira hasa ukizingatia kwamba kwa sasa tunakwenda kucheza tukiwa hatuna presha kubw kama ilivyokuwa mwanzo.

Presha ilikuwa kubwa kwa kuwa tulikuwa nyumbani na kila mmoja matarajio yake ilikuwa kuona tunashinda tena kwa idadi kubwa ya mabao.

Moja ya sehemu ya matokeo kwenye mpira ukiachana na kushinda ama kupoteza na sare pia ni aina ya matokeo japo si matokeo yanayopendwa sana na mashabiki pamoja na benchi la ufundi.

Mwalimu yoyote yule duniani anapopeleka timu uwanjani hesabu zake ni kuona timu inapata matokeo chanya ambayo ni ushindi.

Rai yangu kwa watanzania wote kwa sasa kushikamana na kuungana kwa ajili ya kuiombea timu yetu ya Taifa ikafanye vizuri kwenye mchezo wa marudio ambao utafanyika nchini Kenya.

Agosti 4 sio mbali na siku zinakwenda kasi hivyo mashabiki tuendelee kuwa mstari wa mbele kuipa sapoti timu yetu ambayo inapambana kupeperusha Bendera ya Taifa.

Muda wetu wa kufikia mafanikio kwa sasa ni kwenye mchezo wetu wa marudio na tuna imani nafasi ya kufanya vizuri ipo na inawezekana kabisa.

Jambo la msingi ni kuona sasa namna gani tunaweza kujipanga upya hasa kwa kufanyia kazi yale makosa ambayo tumeyafanya mchezo wa kwanza.

Mchezo wa pili utakuwa na ushindani na kila mmoja anahitaji matokeo ila haimaanishi kwamba itakuwa kazi nyepesi kupata matokeo kikubwa ni imani na kupambana kutafuta matokeo.

Furaha ya watanzania kwa sasa ipo mikononi mwa wachezaji ambao jukumu lao ni kupambana kupata matokeo chanya.

Mashabiki wapeni sapoti vijana wetu wa timu ya Taifa kama ambavyo mmefanya kwenye mchezo wa kwanza.

Tags:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.