KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amempa majukumu mazito kipa wake, Metacha Mnata kuhakikisha anamaliza kila mechi yao bila ya kufungwa ‘clean sheet’.
Kocha huyo ameweka wazi hilo baada ya kumtumia Metacha kama kipa wake namba moja mbele ya Mkenya Farouk Shikalo.
Chini ya Eymael, Metacha aliyejiunga na Yanga akitokea Mbao amecheza mechi tano mfululizo dhidi Singida wakashinda 3-1, Prisons 2-0, Mtibwa Sugar 1-0, Lipuli FC 2-1 na Ruvu Shooting 1-0.
Eymael ameliambia Championi Jumatano, kuwa anafurahia kuona timu yake ikimaliza mechi bila ya kufungwa hivyo ni jukumu la kipa huyo kuhakikisha kwamba haruhusu bao. “Ni kitu kizuri kuona tunaendelea kupata ushindi na pointi muhimu katika kila mechi yetu.
“Lakini kitu ambacho nakitaka kwa sasa ni kupunguza idadi ya mabao ambayo tunafungwa. Ninataka kuona tunamaliza mechi bila ya kufungwa, hivyo ni muhimu kwa safu ya ulinzi na kipa Metacha kujipanga vizuri katika kila mechi yetu,” alisema Eymael
Post a Comment