Baada ya kikiso cha Simba kuonesha kiwango kilicho butu katika mechi za hivi karivuni, inaelezwa kuwa mabosi wa Simba wapo kwenye mchakato wa kusaka Kocha mwingine.
Timu hiyo inayonolewa na Sven Vandenbroeck ambaye ni raia wa Ubelgiji, imekuwa ikipata matokeo ya kusuasua tangu aanze kuinoa jambo ambalo limeanza kuleta wasiwasi katika mechi za ligi na mashindano ya kimataifa hapo baadaye.
Tetesi zilizopo hivi sasa ni kuwa mabosi Simba wanatajwa kutaka kumleta Kocha wa As Vita, Jean Florent Ibenge ili kuchukua majukumu ya Sven.
Taarifa za ndani zinasema uwezekano mkubwa wa Sven kufutwa kazi upo kutokana na uongozi wa juu, mashabiki na hata wanachama kutofurahishwa na namna mwenendo wa timu hiyo unavyoenda hivi sasa.
Sven alichukua nafasi ya kuinoa Simba baada ya kufutwa kazi kwa Patrick Aussema aliyekuwa akiinoa timu hiyo
Post a Comment