Kocha wa Klabu ya Yanga, Luc Eymael, amesema kuwa kulikuwa na harufu kali na isiyoeleweka katika vyumba vyao vya kubadilishia nguo juzi Jumatano, Februari 6, 2020, katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam wakati mechi yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Lipuli FC.
Yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Lipuli, mabao ya Yanga yakifungwa na Mapinduzi Balama dakika ya 14 pamoja na Bernard Morrison dakika ya 31 huku bao la kufutia machozi la Lipuli likifungwa na David Mwassa dakika ya 58.
“Nimeona kipindi cha kwanza kizuri cha Yanga, tulipaswa kufunga magoli matatu au manne…..” alisema Luc.
Aidha, Kocha wa Lipuli Julio Ellieza alisema; “Wametunyima goli dhahiri shahiri, mpira kipa kadakia ndani…. mwamuzi kautoa kuwa kona.”
“Tumefanya makosa, tumeadhibiwa, tunakubali tumefungwa,” alisema Nahodha wa Lipuli FC, Paul Nonga na kuongeza kuwa mpango wao wa kipindi cha kwanza ulifeli ndiyo maana wakafungwa.
Yanga sasa imefikisha pointi 34 baada ya kucheza mechi 17 huku Lipuli ikisaliwa na pointi zake 25 baada ya kucheza mechi 19
Post a Comment