UONGOZI wa Klabu ya Simba umeendelea kumng’ang’ania kipa wa Yanga, Ramadhani Kabwili kutaka kuthibitisha kauli yake ya kudaiwa kutaka kuhongwa gari aina ya IST.
Kabwili katika mahojiano yake na chombo kimoja cha habari nchini, alieleza kuwa kuna kiongozi mmoja wa Simba alimtaka afanye kosa ili apewe kadi ya njano na kukosa mchezo wa watani wa jadi kisha apewe gari aina ya Toyota IST, jambo lililozua sintofahamu.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Katibu Mkuu wa Simba, Arnold Kashembe alisema wanamtaka kipa huyo athibitishe kauli yake aliyoitoa juu ya shutuma katika klabu hiyo huku akidai kuwa, jambo hilo siyo mara ya kwanza kwa Yanga kutoa shutuma kwa Simba na kufikisha taarifa Bodi ya Ligi na TFF.
“Simba bado tunasisitiza Kabwili athibitishe kauli yake, tulilifikisha jambo hili Takukuru ambao tumewaandikia barua pamoja na TFF na Bodi ya Ligi waweze kufanyia kazi jambo hili.
“Hii siyo mara ya kwanza kutokea kwetu, msemaji wa Yanga aliwahi kutoa maneno ambayo si sahihi na tuliwaandikia barua Bodi ya Ligi na TFF kushitaki lakini ikawa kimya, hivyo tumeandika tena kwani jambo hili siyo dogo linalenga kuzichafua taasisi hizo kuwa hazisimamii vyema mpira wa nchi hii,” alisema Kashembe.
GOLI la KAGERE Kwa NAMUNGO, ‘MAHAKAMA’ Yaingilia KATI – “OFFSIDE
Post a Comment