FRANCIS Baraza, Kocha wa Biashara United amesema kuwa wachezaji wake wana morali kubwa na ana imani watasepa na pointi tatu mbele ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Biashara United ipo nafasi ya 9 ikiwa na pointi 31 itamenyana na JKT Tanzania iliyo nafasi ya 7 ikiwa na pointi 34 zote zimecheza mechi 22.
Baraza amesema:" Wachezaji wana morali na ni matumaini yetu kuona kwamba tunapata pointi tatu mbele ya mpinzani wetu kikubwa mashabiki watupe sapoti,".
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.