KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa matatizo ya kikosi chake kwa sasa ni madogo na atayafanyia kazi.
Zahera amesema kuwa kwa sasa anakisuka kikosi imara ambacho kitaleta ushindani msimu ujao kama ambavyo aliahidi msimu uliopita.
"Ninapenda kuona wachezaji wakipambana kwa juhudi ila tatizo lao nimegundua linatokana na kushindwa kukaa kwa muda mrefu hasa kwenye mazoezi.
"Msimu ujao sasa nimepanga kusuka kikosi imara ambacho kitaleta ushindani mwanzo mwisho na mashabiki wenyewe watapenda," amesema.
Miongoni mwa wachezaji ambao wametambulishwa jana ni pamoja na Patrick Sibomana ambaye alifunga bao la kusawazisha kwenye mchezo dhidi ya Kariobangi Sharks, Juma Balinya, Mapinduzi Balama, Ally Ally, Mohamed Banka.
Post a Comment