PEP Guardiola, Meneja wa Manchester City amekuwa wa kwanza msimu huu kuonyeshwa kadi ya njano kwa mameneja ambao wanafundisha Ligi Kuu England.
Guardiola ameonyeshwa kadi hiyo jana kwenye mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Liverpool baada ya kulalamika kuhusu changamoto za Joe Gomez.
Meneja huyo mwenye umri wa miaka 48 hakupendezwa na vitendo vya Liverpool ila baada ya kuonyeshwa kadi ya njano na Martin Atkinson alitulia.
Kadi za njano na nyekundu zimeanza kutumika kwa Mameneja tangu msimu wa 2018/19.
"Mameneja na makocha wanapaswa kuwa mfano kwenye tabia na wanapaswa wawe mfano mzuri kwa wale wanaowaongoza, kuonyeshwa kadi nyekundu ama njano ni sawa wanapokosea," inasomeka taarifa rasmi ya Premier League kuhusu uamuzi huo.
Licha ya kadi hiyo ya njano, Manchester City alitwaa taji lao la kwanza msimu huu kwa kuwafunga wapinzani wao Liverpool kwa mikwaju 5-4 ya penalti baada ya dakika tisini kutoka sare ya kufungana bao 1-1.
Post a Comment