JURGEN Klopp, Meneja wa Liverpool anaamini kuwa msimu ujao ataleta changamoto kubwa mbele ya Manchester City kupigania ubingwa wa Ligi Kuu England.

City ambao ni Mabingwa wapya wa ngao ya jamii baada ya kushinda mbele ya Liverpool jana kwa penalti 5-4 baada ya sare ya kufungana bao 1-1 ndio Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England.

Msimu uliopita, Liverpool ambao ni mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya waliishia nafasi ya pili wakiwa na jumla ya pointi 97.

Ilishinda jumla ya michezo 30 kati ya 38 ya Premier League na ilipoteza mchezo mmoja mbele ya Manchester City. 


"Tuna muda mkubwa na nafasi nzuri ya kujiboresha kwa ajili ya msimu ujao," amesema.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.