TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo imesonga mbele hatua inayofuata ya michuano ya Chan baada ya kushinda mbele ya Kenya.

Dakika tisini zilikamilika kwa timu zote kutoshana nguvu na kuamuliwa kwenda kwenye mikwaju ya penalti.

Tanzania imeshinda kwa penalti 4 huku Kenya ikipachika penalti 1 .Mlinda mlango Juma Kaseja leo amepangua penalti mbili huku kwa upande wa Stars wapachika mabao wakiwa ni Erasto Nyoni,Paul Godfrey, Gadiel Michael na msumari wa mwisho ukikomelwa na Salim Aiyee.

Mchezo unaofuata Kwa Stars ni dhidi ya Sudan katika hatua ya pili kabla ya kufuzu michuano hii moja Kwa moja.

Tags:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.