SIMBA wameamua kurejesha kwa jamii, ambapo kuelekea kwenye SpotiPesa Simba Wiki mashabiki wameanza kujitolea kwa jamii.
Mashabiki wameanza kujitoa kwa kutoa damu sehemu mbalimbali na zoezi hilo lilianza jana stendi ya Mbagala na Ubungo na leo linaendelea pia makao makuu ya klabu pamoja na Mbagala.
Leo Jumamosi Makao Makuu ya klabu Kariakoo na stendi ya Mbagala kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni utakuwa ni mwendelezo wa kuchangia damu.
Pia mashabiki wanawake wa Mwanza jana walitembelea hospitali mbalimbali jijini humo ili kutoa misaada.
Post a Comment