FRANCIS Kahata, kiungo mshambuliaji wa Simba amesema kuwa ubora wa kikosi cha Simba utawapa furaha mashabiki msimu ujao kwenye kila mchezo.
Kahata amejiuga na Simba kwa kandarasi ya miaka miwili akitokea Gor Mahia kwa sasa anaungana na mchezaji mwenzake wa zamani Meddie Kagere.
"Tumefanya kambi nzuri nchini Afrika Kusini na maandalizi yalikuwa safi, kurejea kwetu na kuanza kujipanga kwa ajili ya msimu ujao ni mwendelezo wa burudani.
"Mashabiki waendelee kutoa sapoti kwa timu kwani kazi kubwa iliyo mbele yetu ni kufanya vizuri katika kila mchezo ambao tutacheza," amesema.
Agosti 6, Simba itamenyana na Power Dynamo mchezo wa kirafiki ambao ni maalumu kwa ajili ya kutambulisha wachezaji pamoja na jezi.
Post a Comment