ROMELU Lukaku, mshambuliaji wa Manchester United amesema kuwa kwa sasa anafikiria kutua timu moja wapo ambayo inashiriki Serie A kati ya Juventus ama Inter Milan.

Kaka yake na Lukaku, Jordan amejiunga na Lazio mwaka 2016 jambo ambalo linatajwa kuwa sababu ya yeye kutaka kujiunga huko na amekuwa akijifunza lugha ya kiitaliano.

Lukaku amesema: "Kaka yangu anacheza Italia, nimekuwa nikitazama michezo yake mingi nimependa namna ilivyo na wanavyozungumza.

Inter Milan walikuwa mstari wa mbele kuipata saini yake ila inaelezwa dili lilibuma na sasa anazungumza na Juventus.

Juventus wapo tayari kumuacha Paulo Dybala kwenda Manchester United ndani ya Uwanja wa Old Trafford kama sehemu ya dili la Lukaku.

United imesema thamani ya Lukaku ni pauni Milioni 75 na hawapo tayari kushusha dau hilo.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.