KAIMU Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Suleman Matola amesema ni wajibu wa watanzania kuenedelea kuipa sapoti timu ya Taifa kuelekea mchezo wa Kenya kwani nafasi ya kupenya ipo.

Kwenye mchezo wa kwanza wa kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya Chan inayotarajiwa kufanyika nchini Cameroon, 2020 uliopigwa uwanja wa Taifa, Stars ilikubali kupata sare ya bila kufungana.

Matola amesema: "Huu ni mwanzo kwa wachezaji kwani ilikuwa ni mechi ngumu na yeynye ushindani, kwa sasa tunaachana na matokeo yaliyopita tunatazama wakati ujao ambao ni mchezo wetu muhimu kuliko uliopita.

"Makosa yetu tumeyafanyia kazi hivyo mashabiki na watanzania kiujumla watupe sapoti kuelekea mchezo wetu wa marudio imani bado ipo," amesema.

Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Agosti 4 nchini Kenya na ili kufuzu michuano hii ni lazima Stars ishinde.

Tags:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.