ABDULHARIM Humud nyota mpya wa Mtibwa Sugar amesema kuwa kikubwa kinachowabeba kwenye mechi za kirafiki ni kufuata maelekezo ya mwalimu na juhudi.
Mtibwa Sugar kuelekea kwenye maandalizi ya Ligi Kuu Bara wamezidi kunoga kwa kucheza mechi za kirafiki bila kupoteza kwani walishusha kichapo cha mabao 10-0 hivi karibuni.
Mchezo wao wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Burundi, Aigle Neir FC uliochezwa uwanja wa Chamazi walilazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 kabla ya kushusha kichapo cha mabao 10-0 mbele ya Moro Combine mchezo uliochezwa uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Jana waliibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya KMKM uwanja wa Manungu.
Post a Comment