NICOLAS Pepe, amesaini kandarasi ya miaka Mitano ndani ya Arsenal kwa dau la pauni milioni 72 akitokea klabu ya Lille.
Pepe anakuwa nyota wa nne kusaini ndani ya Arsenal msimu huu, msimu uliopita alitupia jumla ya mabao 23 katika michezo 41 aliyocheza.
Jumanne ya wiki hii alikamilisha masuala ya vipimo jijini London kabla ya kusaini kandarasi mpya ya miaka mitano.
Ana umri wa miaka 24 na amezaliwa nchini Ufaransa lakini anakipiga kwenye timu ya Taifa ya Ivory Coast anaingia kwenye rekodi ya wachezaji ghali ndani ya Arsenal akimpoteza Pierre Aubameyang ambaye ada yake ilikuwa pauni milioni 55 mwaka 2018.
Unai Emery, Meneja wa Arsenal amesema "Nicolas ni miongoni mwa wachezaji wenye vipaji na uwezo wake unahitajika ndani ya timu Bora .
"Kupata saini ya winga makini ni miongoni mwa malengo yetu hasa kwenye msimu huu wa usajili ndio maana amejiunga nasi," amesema.

Post a Comment