UONGOZI wa Yanga, umemtaka Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Almas Kasongo kuanza kuiweka sawa ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo wanadai bado haipo vizuri ili kuepusha malalamiko yasiyo ya lazima kutoka kwa klabu mbalimbali.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, amesema kuwa wao kama uongozi wanampongeza Kasongo kwa kupewa nafasi hiyo na kudai kuwa yeye ana uzoefu wa soka la nchi hii na anajua mambo mengi, hivyo atumie uzoefu wake kutatua matatizo yanayojitokeza mara kwa mara hasa katika upangaji wa ratiba ya ligi kuu.
Kasongo amekuwa bosi mpya wa Bodi ya Ligi akichukua nafasi ya Boniface Wambura ambaye kwa sasa amekuwa Mkurugenzi wa Habari na Masoko wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Akizungumza na Spoti Xtra, Mwakalebela alisema kuwa wanamuamini Kasongo
Post a Comment