HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa Ruvu Shooting wasitarajie kuokota dodo chini ya mbuyu kesho Uwanja wa Taifa kwa kuwa mchezo wa kwanza walishinda kwa kubahatisha.
Yanga ilipokuwa chini ya Mwinyi Zahera, mechi ya kwanza ya mzunguko wa kwanza msimu huu iliyochezwa Uwanja wa Uhuru ilifungwa bao 1-0 na Ruvu Shooting ambayo kesho Februari, 8 itakutana nao tena.
Bumbuli amesema:-"Mwanzo kweli walitufunga na tuliacha pointi tatu, pale walibahatisha wasitarajie tena kuokota dodo chini ya Mbuyu hilo halipo kwa sasa tuna mpango mwingine kabisa.
"Timu imeanza kuimarika na muunganiko ni imara tutapambana kupata pointi tatu tunajua kwamba wao wanaongea sisi tutafanya kwa vitendo," amesema.
Yanga ipo chini ya Luc Eymael kwa sasa mchezo wake wa hivi karibuni ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Lipuli na Ruvu Shooting nao walishinda bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar.
Post a Comment