UONGOZI wa Yanga umesema kuwa mpira sio sawa na rede una kanuni zake jambo ambalo wanapaswa walielewe mashabiki.
Yanga imelazimisha sare kwenye mechi nne mfululizo za Ligi Kuu Bara na kupoteza pointi nane kati ya 12 ilizokuwa inazisaka.
Ilianza kupata sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Mbeya City kisha ikafuata 0-0 mbele ya Tanzania Prisons, 0-0 mbele ya Polisi Tanzania na sare ya 0-0 mbele ya Coastal Union.
Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema:-"Mpira una kanuni zake na kila timu inapambana kupata matokeo chanya, hivyo nasi tunapambana, Mpira sio sawa na rede. timu zinacheza, mashabiki waendelee kuipa sapoti timu.
Yanga imefunga mabao mawili kwenye mechi zake nne mfululizo ikiwa imefunga jumla ya mabao 25 baada ya kucheza mechi 22.
Post a Comment