Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck amefurahia ujio wa viungo wake washambuliaji, Luis Miquissone na Shiza Kichuya akiamini utaiboresha safu yake ya ushambuliaji.

Kauli hiyo aliitoa juzi mara baada ya kiungo wake Kichuya kupata kibali cha kucheza soka (ITC) kabla ya Luis kupata chake juzi baada ya timu hiyo kupeleka taarifa za wachezaji hao kwenye Kamati ya Hadhi ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Wachezaji waliojiunga na Simba katika usajili wa dirisha dogo tayari wamepewa vibali, hivyo wataanza kuonekana katika michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara na mashindano mengine.

Sven alisema kuwa, anaamini uwezo wa viungo hao wanaompa matumaini ya kuiboresha safu yake ya ushambuliaji ambayo mara kadhaa amekuwa akiilalamikia kutokana na kushindwa kutumia nafasi nyingi ambazo wanazipata.

Sven alisema ameahidi kuwapa nafasi mastaa hao katika michezo ijayo ya ligi baada ya kuridhishwa na viwango vyao katika mazoezi yake tangu wamejiunga na timu.

“Suala la kucheza au kutocheza lipo chini na nitawatumia hao kutokana na aina ya mchezo nitakaokutana nao, hivyo ni matarajio yangu kuona wakiipambania timu uwanjani.

“Sina shaka na uwezo wa viungo wangu Kichuya na Luis, ni suala la muda tu wao kucheza katika timu na kikubwa ninataka kupambana kila wanapopata nafasi ya kucheza katika timu.

Nyota hao walianza kuonyesha makeke kwa mara ya kwanza Uwanja wa Uhuru mchezo wa ligi dhidi ya JKT Tanzania ya Mohamed Abdallah

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.