Ile tabia ya baadhi ya wachezaji na makocha kuwadharau waandishi wa habari kuhusiana na suala la mahojiano imemtokea puani nahodha wa Azam FC, Aggrey Morris.
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Februari 10, 2020 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya uamuzi ufuatao;
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Februari 10, 2020 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya uamuzi ufuatao;
Mechi namba 189:Azam Fc 1 vs Tanzania Prisons Fc 1
Morris amepigwa faini ya kiasi cha Tsh 200,000/=(Laki Mbili) kwa kosa la kugoma kuongea na waandishi wa habari mara baada ya mchezo kumalizika katika mechi iliyochezwa Februari 05,2020 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Adhabu hii imetolewa kwa mujibu wa Kanuni namba 38(18) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji
Post a Comment