PHIONA Nabbumba wa Timu ya Wanawake chini ya miaka 20 ya Uganda alijichanganya dakika ya 48 ya kipindi cha pili kuitungua timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20, 'Tanzanite' kwenye mchezo wa pili wa kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia.

Dakika 11 ziliwatosha Vijana wa Tanzanite kuandika bao la kwanza la kuweka mzani sawa kupitia kwa Diana Msemwa aliyepachika bao hilo dakika ya 59.

Mambo yalizidi kunoga kwa Wadada hao ambapo dakika 9 mbele wakapachika mbao mwingine wa pili kupitia kwa Opa Clement dakika ya 68 uliopindua meza kibabe.

Ushindi huo unawatosha kabisa Tanzanite kusonga mbele kuendelea mchakato wa kutafuta tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia linalotarajiwa kufanyika mwezi Julai.

Tanzanite inapenya kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-2 baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa kushinda mabao 2-1.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Startimes huko nchini Uganda na vijana hao walio chini ya Bakari Shime waliibuka wababe.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.