UONGOZI wa Simba umesema kuwa umefungwa na timu iliyokuwa bora ndani ya Ligi Kuu Bara.

Simba ilifungwa bao 1-0 na JKT Tanzania kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Uhuru, jana, Februari 7,2020 lililopachikwa kimiani na Adam Adam dakika ya 24 lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wamefungwa na timu iliyokuwa bora ndani ya uwanja.

"Tumefungwa na timu bora, hakuna cha kukata tamaa bado mapambano yanaendelea,".

Simba imepoteza jumla ya mechi mbili ndani ya ligi kati ya 20 ambazo imecheza kwa sasa na zote imepoteza kwa kufungwa bao moja.

 Iliianza kufungwa mbele ya Mwadui FC bao 1-0 mzunguko wa kwanza na safari hii imefungua mzunguko wa pili kwa kichapo cha bao 1-0 mbele ya JKT Tanzania

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.