LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa Tanzania inahitaji ligi yenye ushindani ili kupata wachezaji bora watakaounda timu ya taifa imara.
Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa ameona tatizo lipo kwenye mechi nyingi ambazo anacheza pamoja na zile anazozitazama kutokuwa na ushindani mkubwa jambo ambalo linaleta upinzani kwa timu chache zenye nguvu.
"Unajua ukitaka kuwa na timu bora ya taifa ni lazima uwe na ligi imara ambayo ina ushindani kwa muda ambao nimetazama ligi ya hapa kuna matatizo ambayo yanapaswa yafanyiwe kazi, kuanzia maamuzi na namna wachezaji ambavyo watakuwa wanafanya ndani ya uwanja.
"Timu nyingi zinacheza vizuri lakini si kwa kiwango ambacho kinatakiwa ni lazima ligi iwe imara na kukiwa na ligi imara kutakuwa na timu bora ya taifa
Post a Comment