JANUARI wengi wanapenda kuuita mwezi dume kutokana na kuwa na majalada mengi ambayo yamechanganywa sehemu moja ila ghafla tu umemeguka na sasa ni Februari.
Kwenye ulimwengu wa michezo, Ligi Kuu Bara inazidi kumeguka taratibu ambapo kila kocha anapambana kuweka rekodi zake kwa kuwapa majukumu wachezaji wake kufanya kile alichowaelekeza.
Vita kubwa kwa sasa ni ubora na tuzo kwa Kocha bora na mchezaji bora ndani ya Ligi Kuu Bara kutokana na rekodi zao ambazo wameziweka mwezi Januari.
Cheki namna balaa la makocha na wachezaji waliozibeba timu ndani ya mwezi Januari ambao habari yake tayari imeshaandikwa namna hii:-
Azam FC
Arstica Cioaba wa Azam FC, Januari ameongoza timu yake kwenye mechi tano ameshinda nne na sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar.
Safu yake ya ushambuliaji imefunga mabao 9, safu ya ulinzi inayoongozwa na Nicolas Wadada imeruhusu mabao matatu ya kufungwa.
Wachezaji waliofanya vizuri ndani ya Azam ni Wadada mwenye jumla ya pasi sita za mabao ila mwezi Januari alitoa pasi moja na Idd Chilunda aliyetupia mabao mawili Januari.
Matokeo yake yapo namna hii:-Singida 1-2 Azam Fc,
Azam 2-0 Lipuli, Azam 1-0 Yanga, Mwadui 0-1 Azam, Azam Fc 3-1 Friends, huu ulikuwa ni wa Kombe la Shirikisho.
.
Simba
Sven Vandenbroeck, Januari ameongoza timu yake mechi tano na ameshinda nne sare moja ya kufungana mabao 2-2 na Yanga.
Dilunga Januari alifunga mabao matatu sawa na Meddie Kagere pia alitoa pasi moja ya bao. Simba imefunga jumla ya mabao 11 na kuruhusu mabao manne ya kufungwa.
Matokeo yake:-Simba 2-2 Yanga , Mbao 1-2 Simba, Alliance 1-4 Simba, Simba 2-1 Mwadui huu ulikuwa ni mchezo wa Kombe la Shirikisho, Simba 3-2 Namungo.
Pointi 12 alizokuwa anazisaka Sven ameambulia 10.
Yanga
Luc Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga raia wa Ubelgiji, mwezi Januari ameongoza timu kwenye jumla ya mechi nne amepoteza mbili na kushinda mechi mbili.
Bernard Morrison ni mchezaji ambaye alifanya maajabu ndani ya mwezi Januari alitoa pasi moja ya bao mbele ya Singida United lilifungwa na Haruna Niyonzima, Yikpe kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho ambapo pia alifunga mbele ya Tanzania Prisons. Yanga imefunga jumla ya mabao matano na kufungwa mabao matano.
Matokeo yapo hivi:Yanga Sc 0-3 Kagera Sugar, Azam 1-0 Yanga , Singida 1-3 Yanga
Yanga 2-0 Prisons ilikuwa ya Kombe la Shirikisho
Yanga 2-0 Prisons ilikuwa ya Kombe la Shirikisho
Kwenye pointi tisa alizokuwa anaziwinda Luc amekusanya tatu.
Coastal Union
Juma Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union, Januari ameiongoza timu yake kwenye mechi tatu na imeshinda mechi mbili na kulazimisha sare moja.
Safu ya ushambuliaji iliyo chini ya Ayoub Lyanga ambaye alifunga mabao mawili Januari imefunga jumla ya mabao matatu kwenye mechi tatu na kufungwa mabao mawili. Matokeo yao yapo namna hii:-Coastal 1-0 Tanzania Prisons,Coastal 1-0 Kagera, Coastal 1-1 Biashara.
Coastal Union kwenye pointi tisa ilizokuwa inasaka imekusanya saba.
Namungo
Namungo ya Hitimana Thiery, Januari imecheza mechi nne imeshinda tatu na kupoteza mechi moja.
Safu ya ushambuliaji chini ya Relliants Lusajo aliyefunga mabao matatu Januari, imefunga jumla ya mabao 10 na kufungwa mabao nane.
Matokeo yake :-Mbeya City 2-3 Namungo, T.Prisons 2-3 Namungo, Namungo 2-1 Biashara ulikuwa ni wa Kombe la Shirikisho, Simba Sc 3-2 Namungo.
Namungo kwenye jumla ya pointi tisa imekusanya sita
Post a Comment