LIONEL Messi, mshambuliaji na nahodha wa Klabu ya Barcelona imeelezwa kuwa yupo kwenye hesabu za kutua ndani ya Klabu ya Manchester City inayoshiriki Ligi Kuu England.
Uongozi wa Barcelona ukiongozwa na Eric Abidal ulikaa na rais wa Barcelona Josep Bartomeu jana Jumatano kwa muda wa masaa mawili kujadili suala hilo ambalo limeanza kupewa uzito.
Inaelezwa kuwa Messi kwa sasa anataka kupata changamoto mpya kwa kuondoka kwenye ufalme wake wa La Liga ambapo amedumu kwa muda mrefu.
Mkataba wa Messi unameguka mwaka 2021 ndani ya Barcelona na inaelezwa kuwa anaweza kuondoka mwishoni mwa msimu endapo atakuwa hana furaha ndani ya timu hiyo.
Messi mwenye miaka 32 anaamini kuwa kujituma kwake ndio chanzo chake kufika hapo alipo na miongoni mwa timu ambazo anapenda kuzitumikia ndani ya England ni Manchester City

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.